Jumatatu 20 Oktoba 2025 - 07:35
Mahdawiyyah katika Qur’ani (Sehemu ya Tatu)

Hawzah/ Baadhi ya aya katika Qur’ani Tukufu zinahusiana na ushindi wa wenyekudhoofishwa dhidi ya wenye nguvu, na zinabainisha kwamba hatimaye dunia itakuwa ya wale wanaostahiki — yaani wacha Mungu na wafuasi wa haki.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, mfululizo wa utafiti kuhusiana na Mahdawiyyah kwa anuani ya “Kuielekea Jamii Bora” umetolewa kwa lengo la kueneza mafundisho na maarifa yanayohusiana na Imam Mahdi (aj) kwa wasomi na wapenda elimu.

Aya ya Pili

«وَنُریدُ أنْ نَمُنّ عَلَی الّذینَ اسْتُضْعِفُوا فِی الارْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أئمّْة وَنَجْعَلَهُمُ الْوارِثینَ.»

“Sisi tunataka kuwafadhili wale waliodhoofishwa katika ardhi, na tuwafanye wawe viongozi na warithi wa dunia.”
(Surat al-Qasas (28), Aya ya 5)

Aya hii, kwa mujibu wa maneno ya Imam Ali (as) katika Nahjul-Balagha na mapokezi mengine kutoka kwa Maimamu wengine (as), inazungumzia ushindi wa wanyonge dhidi ya wenye nguvu, na kwamba mwisho wa dunia utakuwa wa wale wanaostahiki.

Aya hii haizungumzii tu mpango maalumu uliowahusu Wana wa Israil, bali inaelezea kanuni ya jumla ya kihistoria kwa vizazi vyote na zama zote — bishara ya ushindi wa haki juu ya batili, na imani juu ya ukafiri.

Mfano wa awali wa utekelezaji wa aya hii ni serikali ya Mtume Muhammad (saww) na maswahaba wake baada ya kuenea Uislamu.

Mfano mpana zaidi na kamili kabisa ni kuonekana serikali ya haki na uadilifu duniani kote kwa mkono wa Imam Mahdi (aj).

Aya hii ni miongoni mwa zile zinazotoa bishara ya uwazi kabisa kuhusiana na “kuonekana kwa serikali hiyo”, na kwa sababu hiyo, Ahlul-Bayt (as) wametaja wazi katika tafsiri zao kuwa aya hii inamhusu Imam Mahdi.

Imam Ali (as) katika Nahjul-Balagha anasema:

«لَتَعْطِفَنَّ الدُّنْیا عَلَینَا بَعْدَ شِمَاسِهَا عَطْفَ الضَّرُوسِ عَلَی وَلَدِهَا وَ تَلَا عَقِیبَ ذَلِکَ "وَ نُرِیدُ أَنْ نَمُنَّ عَلَی الَّذِینَ اسْتُضْعِفُوا فِی الْأَرْضِ وَ نَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَ نَجْعَلَهُمُ الْوارِثِینَ".»

“Dunia, baada ya ukaidi na uasi wake — kama ngamia anayekataa kumpa maziwa anayedonya bali anayahifadhi kwa mtoto wake — itatuelekea sisi kwa upole... 
Kisha Imam alisoma aya hii:

‘Na tunataka kuwafadhili wale waliodhoofishwa katika ardhi...’.”
(Nahjul-Balagha, Hikma ya 209)

Hadithi nyingine kutoka kwa Imam Ali (as)

«هُمْ آلُ مُحَمَّدٍ یبْعَثُ اللَّهُ مَهْدِیهُمْ بَعْدَ جَهْدِهِمْ فَیعِزُّهُمْ وَ یذِلُّ عَدُوَّهُمْ.»

“Hao ni Ahlul-Bayt wa Muhammad (sawww). Mwenyezi Mungu atamleta Mahi wao (Imam Mahdi) baada ya mateso na mashinikizo waliyopewa, kisha atawaenzi wao na kuwadhalilisha maadui zao.”
(Sheikh al-Tusi, Kitab al-Ghaybah, uk. 184)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho: “Darsname-ye Mahdawiyyat” kilichoandikwa na Khoda-Morad Salimiyan, huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha